NJIA ZA KUSIMAMISHA GARI LILILOFELI BREKI MWENDONI.

1

Ili kujiandaa na kujua jinsi ya kufanya pale breki ya gari yako imeshindwa kufanya kazi wakati unaendesha, nakukaribisha katika kozi hii. Pia kuna vidokezo vya kuzuia breki kushindwa kufanya kazi.

2

UTANGULIZI: Hali isiyowezekana, bado inaweza kutokea. Ni muhimu kujua jinsi ya kuchukua uamuzi breki zitakaposhindwa kufanya kazi. Uamuzi wa mgawanyiko wa pili unaweza kuokoa maisha.

3

Gari zenye Manual Gearbox. Gari zenye manual gearbox inaweza kua rahisi kidogo lakini watumiaji wa hizi gari sio wengi. Kwa gari hili utasimama kupitia kushusha gear za chini, breki kwa injini.

4

Kama uko gear ya nne shuka tatu, achia clutch taratibu, kanyaga tena clutch weka gear ya pili. Achia clutch taratibu alafu ukanyage tena uweke gear ya kwanza. Kisha vuta handbrake taratibu.

5