Ewe KIJANA ijue AfyaYa Akili, Na changamoto Kisaikolojia!

1

Mpendwa KIJANA, Je unajua afya ya akili ni nini? Magonjwa ya akili je? Chanzo cha magonjwa ya akili? Changamoto za kisaikolojia? Utajuaje unahitaji msaada wa kisaikolojia? Utatunzaje afya yako ya akili?

2

Matatizo ya afya ya akili, changamoto za kisaikolojia na magonjwa yake yanaweza kutokea kwa mtu yeyote na mda wowote, kwa watu wa kila kizazi, rangi, dini, na tabaka na rika lolote katika jamii.

3

Changamoto za afya ya akili kwa vijana ni dharula hivo kutoa elimu na huduma za afya ya akili kwa vijana zinahitajika kidharula ili kujifunza zaidi namna bora ya kudumisha afya zao za akili.

4

Tunashuhudia vijana wakisitisha uhai wao (suicide), vijana wenye umri kati ya miaka 15-29. Karibu nusu ya magonjwa ya akili huanza kabla ya umri wa miaka 14.

5