KWA NINI MBU HUPENDA KUPIGA KELELE SIKIONI?

1

Je! Unakerwa na kelele za Mbu sikioni? Ule mlio wake wa Ziiiziii. Simulizi hii kutoka "Nchi ya Mabawa" inakujuza sababu ya Mbu kupenda kupiga kelele sikioni na namna ya kuiondosha hali hiyo.

2

Hapo zamani za kale sikio alikuwa ni msichana mrembo sana. Alisifiwa na kila mtu katika nchi aliyokuwa akiishi. Kila kijana wa kiume aliyesikia sifa za sikio alitamani awe mchumba wake.

3

Wale waliofanikiwa kumtia machoni waliajabia uzuri wake na kuwa tayari kufanya chochote ili wampate hata kama ni kuhatarisha maisha yao. Mbali na uzuri wake, vilevile sikio alisifika kwa dharau iliyochupa mipaka hususani kwa vijana wa kiume.

4

Kila mwanamume aliyemfuata alimwambia maneno ya shombo. Wanaume wengi walikata tamaa na kuacha kadari iamue kiumbe atakayemchumbia sikio. “Mimi nataka kumchumbia sikio,” Mbu alisikika akitamba siku moja katika Nchi ya Mabawa.

5