Mambo Makuu 3 Ya Kuzingatia Kabla Ya Kununua Gari

1

Mwisho wa hii kozi fupi, utaweza kupata ufahamu mzuri wa kukusaidia katika uamuzi wa kuchagua gari sahihi kwa matumizi yako.

2

UTANGULIZI. Watu wengi tumekua na dhana pototfu pindi tunapokua tunataka kununua gari; "utasikia mtu anakuuliza, inakula mafuta?"

3

JAMBO LA KWANZA LA KUZINGATIA - Angalia bajeti yako ya pesa. Kupitia kiasi chako cha pesa kitakuongoza katika aina za gari za kiwango chako cha pesa kwasababu bei za gari zinatofautiana.

4

JAMBO LA PILI LA KUZINGATIA - Gari Unanunua kwaajili ya matumizi yapi. Je unanunua gari kwaajili ya familia au binafsi, je gari ambayo utakua ukienda nayo safari za mbali au ni safari za mjini,

5

Je itakayokua ikibeba vitu vizito au kwaajili ya watu pekee. Au pia unachagua gari kwaajili ya kuwa unaitumia kwa mbio mbio.

6

Mafano: 1 Watu wengi wamekua wakinunua Noah kwa familia na pia ya kubebea samani za dukani wakati Noah sio ya kubebea mizigo. Kubebea mizigo Noah Diff yake hua inakufa inakua inatoa mlio.

7

Mfano: 2 Mtu ananunua Passo na anakua anasafiri nayo sehemu za mbali. Kufanya hivyo kunaua sana pump ya mafuta na gear box. Hii inakugharimu sana. Passo ni nzuri sana kwa safari za mjini.

8

47

4

14

3

Comments

Nyayo Zangu

Kabisa, hichi ni kitu ambacho wengi hatuna taarifa nazo, alafu inakuja kutugharmu kiasi kikubwa cha pesa na muda mbele ya safari!!!! Asante sana kutushirikisha!

Lawrence Nyaki

Nakubaliana na hii kauli “Matengenezo ya miguu ya gari yako hua yanagharimu sana kuliko sehemu nyingine ya gari yako“ kwa asilimia mia moja. Watu wengi hatuzingatii hali ya miguu ya magari wakati wa kununua gari.