Kwanini Biashara Hazifanikiwi? (Why do businesses fail?)

1

Katika Somo hili tutajifunza kwa nini hali hii hutokea ili tuweze kuibadilisha na biashara zetu ziweze kufanikiwa.

2

Biashara ni shughuli yoyote halali ambayo mtu anaweza akaifanya kwa lengo la kumuingizia faida. Hata hivyo biashara nyingi huanzishwa lakini hazionekani kuwa na mafanikio.

3

1. KUTOKUTOFAUTISHA SHUGHULI ZA BIASHARA NA MWENYE BIASHARA!

4

Hii ni sababu ya kwanza. Biashara ni kitu tofauti na Mwenyebiashara. Na shughuli za biashara ni tofauti na shughuli za Mwenye biashara (BUSINESS ENTITY CONCEPT).

5

Mwenyebiashara anamiliki biashara, lakini bidhaa za biashara ni za biashara si zake. Hata fedha zinazotokana na mauzo ya bidhaa za biashara si zake bali ni za biashara.

6

Kama ni hivyo, sasa Mwenyebiashara anastahili nini kutoka kwenye biashara?

7

Anastahili kulipwa Mshahara na biashara (na uzuri anajipangia mshahara yeye mwenyewe).Aidha faida inayopatikana kwenye biashara ni ya wote, yeye na biashara yake.

8

Yeye anastahili kiasi kidogo cha faida na kiasi kikubwa ni cha biashara ili kiweze kuongeza mtaji wa biashara. Lakini wengi wetu tunadhani Mwenyebiashara na biashara yake ni kitu kimoja!

9

2. KUFANYA BIASHARA BILA MPANGO WA BIASHARA!

10

Kufanya biashara bila mpango ni sawa na kuitumbukiza mashua juu ya maji na wewe kupanda na kusubiri upepo ukupeleke unakotaka kwenda.

11