Stadi Za Kufanya Mapatano! (Negotiation Skills)

1

Katika mada hii tutajifunza mambo yafuatayo: 1. Maana ya Mapatano. 2. Kwa nini tunafanya mapatano? 3. Hatua za kufuata wakati wa kufanya mapatano yenye tija. 4. Mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya mapatano.

2

UTANGULIZI Binadamu analazimika kufanya mapatano kuhusu mambo mengi katika misha; kwa mfano, wakati wa kufunga ndoa, kuuza na kununua, kutatua ugomvi na hata katika kutofautiana misimamo.

3

1. MAPATANO NI NINI? Mapatano ni mazungumzo na majadiliano baina ya pande mbili au zaidi kwa lengo la kufikia muafaka kwa lile wanalozungumzia.

4

Mapatano yanahusisha uwezo wa kuzungumza, kujenga hoja, kushawishi, kutafsiri lugha za ishara na hata kudanganya.

5

2. KWA NINI TUNAFANYA MAPATANO? Wanyama wanapotofautiana jambo, hupigana na mshindi kupatikana. Lakini binadamu hahitaji kugombana ili kufikia muafaka.Kwa hiyo, kupatana ni jambo la kibinadamu.

6

Tunapatana ili kfikia muafaka na kuzuia ugomvi. Tunapatana ili kuwa na ushirikiano endelevu. Tunapatana ili kuweza kuuza na kununua bidhaa ili kukidhi mahitaji yetu.

7