BIASHARA INAHITAJI USIMAMIZI MZURI

1

Suala la kuwa na biashara ni moja lakini kusimamia hiyo biashara ni jambo lingine.

2

Usimamizi wa biashara ni suala muhimu ambalo kila mjasiriamali anapaswa kulipa kipaumbele ili kuwa na biashara endelevu (Sustainable business).

3

Ukiwa na usimamizi mzuri katika biashara ni rahisi kujua maeneo ambayo haufanyi vizuri (area of weakness) na maeneo ambayo unafanya vizuri (area of strength ).

4

Makampuni makubwa na mashirika huwa wanajifanyia tathimini kujua hali yao ya sasa na kisha kuweka mkakati ambao utawasidia kufanya vizuri.

5

Wewe kama mjasiriamali unahitaji kufanya tathimini ya biashara yako ili kuweza kujua iko katika hali gani?.

6

Watu wengine huwa wanajiuliza na kuchanganyikiwa wakati biashara zao zimekufa au kuanguka katika soko. l

7

Lakini wangekua ni watu wakufanyia tathimini ya biashara zao kuna changamoto wangebaini mapema na kisha kuzitatua.

8

Usimamizi wa biashara ni mchakato unao jumuisha namna biashara inaendeshwa, soko la bidhaa/huduma, usimamizi wa rasimali fedha katika shughuli za utendaji wa biashara.

9

Katika usimamizi wa fedha ndio mahali utapobaini vizuri mapato na matumizi ya biashara yako.

10

Ni eneo ambalo litakupa picha ya utendaji wa biashara (business perfomance) ukiangalia takwimu za mauzo ya biashara yako ninakuambia nini ?

11

Ili uweze kuwa na uwezo wa kufanya tathimini ya masuala ya mauzo ya bidhaa zako na matumizi katika uendeshaji wa biashara ni lazima uwe na utaratibu wa kuweka kumbukukumbu za mauzo na matumizi vizuri.

12

Kila unapofanya mauzo katika biashara yako jitahidi kuweka kumbukumbu vizuri kwasababu ni mtaji wa usimamizi mzuri wa kifedha katika biashara yako.

13

Unapotunza kumbukumbu vizuri zitakusaidia kujua utendaji wa biashara yako kama ni mzuri au la na kisha kufanya maamuzi sahihi.

14