1
Ni shauku ya kila mtu kuwa na biashara yenye uwekezaji mkubwa na miundo mbinu mikubwa lakini kabla ya kuwekeza kwenye eneo lolote anza kuwekeza kwako mwenyewe.
2
Kama unatamani kuwekeza katika kilimo biashara wekeza muda wa kijifunza kwenye hili eneo ujue kilimo biashara kikoje, kinaendeshwaje, kina changamoto gani.
3
Tafuta vikundi vya wakulima na taasisi ambazo zinawajengea uwezo wakulima jiunge nao halafu shiriki kwenye mafunzo mbalimbali hususani yale ya shamba darasa usiache.
4
Tafuta wakulima wanaofanya shughuli hiyo na wafanyabiashara jifunze kwao kwasababu wao wanaujuzi kutoka kwenye wanja wa kilimo hivyo maaarifa yao sio nadharia.
5
Mara nyingi ukiwasikiliza watu ambao wamefanikiwa katika biashara fulani utasikia wakielezea mazuri,
6
faida wanayopata na mafanikio waliyonayo kama unatamani kufanya vizuri kwenye biashara jifunze hao watu walifanikiwaje, walitumia mbinu gani, wanapata changamoto gani na je wanakabiliana nayo vipi?
7
14
4
13
3
Comments