Aina 3 Za Watu Wanaotuathiri Tabia!

1

Tutajifunza: 1. Jinsi tabia zetu zinavyo jengeka 2. Jinsi watu wanavyotuathiri tabia 3. Jinsi ya kujilinda na tabia mbalimbali

2

Kwenye kitabu cha Atomic Habits, mwandishi James Clear anaongelea tabia za wanadamu, na jinsi ya kuondokana na tabia mbaya, na kujenga tabia nzuri.

3

Kwenye kitabu hiki, mwandishi aliongelea aina za watu ambao tunawaiga, na jinsi ambayo kuwaiga watu hawa kuna badilisha tabia zetu.

4

1. Watu Wa Karibu (The Close) Ukizungukwa na watu wenye tabia fulani, basi nawewe utakuwa na hio tabia. Ikitokea watu wanao kuzunguka wana tabia mbaya, nawewe utakuwa hivyo, na kama watu hao wanatabia nzuri nawewe utachukua tabio hio.

5

Kwa mfano, kama uko na watu ambao wanaongea kiingereza kila wakati, basi na wewe unajikuta unaanza kuwa unaongea kiingereza mara kwa mara. Ndio maana wakati wa utotoni, wazazi walikuwa wanapenda kutupeleka vijijini kujifunza lugha.

6

2. Watu Wengi (The Many) Wakati ambapo tukiwa hatuna uhakika na maamuzi gani ya kuchukua, tunajikuta tunaangalia maamuzi ya wale walio wengi.

7

Kwa mfano, kama huna uhakika wa biashara gani ya kuanzisha, basi ni rahisi kuangalia biashara ambazo watu wengi wanafanya.

8