1
Stori fupi ya kuchekesha kuhusu sungura na njaa ya karoti! Simulizi Kutoka "Nchi Ya Mabawa."
2
Siku moja Sungura alikuwa akihisi njaa. Pamoja na kwamba alikuwa na vyakula vya aina mbalimbali ndani ya nyumba yake kama Mahindi, Maharagwe na Kunde, yeye alikuwa anataka Karoti tu.
3
Ilikuwa njaa au hamu? Tufanye ni njaa tu jamani. Maana hata mimi mwenyewe sielewi. Alitoka na kwenda katika duka la ujenzi lililokuwa mita kadhaa kutoka nyumbani kwake.
4
Alipofika alitazama kila pembe ya duka lile, lakini hakuona Karoti. Hakuridhika. Alimsogelea muuzaji. "Samahani. Eti Karoti zipo?" Aliuliza Sungura bila ya wasiwasi huku akimtazama muuzaji usoni.
5
Masikio yalikuwa wima kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa usikivu, lakini pia furaha kuwa anakaribia kupata chakula alo na hamu nacho. "Hivi una akili kweli wewe? Tangu lini Karoti zikauzwa kwenye duka la ujenzi. Sokoni hupajui? Hakuna Karoti hapa. Toka!"
6
Muuzaji alipayuka. Hasira za kuchubuliwa na nondo, vumbi la saruji na kuchomwa na misumari zote alizimalizia kwa Sungura. Sungura aligeuza na kurejea nyumbani kwake kichwa chini. Hata masikio yalilala.
7
Nguvu ya kuyasimamisha angaliitoa wapi ilihali muuzaji alikuwa kamvua nguo. Baada ya siku kadhaa, Sungura alikumbuka tena kula Karoti. Alifunga safari na kurejea kwenye lile duka la ujenzi.
8
Hivi Sungura alikuwa na akili kweli jamani? Alimkuta muuzaji yuleyule, na alimuuliza swali lilelile. "Ukirudi tena hapa siku nyingine. Nitachukua nyundo na misumari halafu nitakusurubisha mtini.
9
40
5
17
3
Comments