NISSAN X-TRAIL T30 (Year 2001 - 2007)

1

Nissan X-Trail T30 ni shujaa alie bambikiwa sifa mbovu na mafundi wasio na weledi. Nakukaribisha katika hii kozi ili uweze kufahamu kwanini ninaiita shujaa.

2

Historia fupi: Nissan X-Trail ilipenyezwa katikati, chini ya Nissan Patrol na juu ya Nissan Terrano. Hii ni mojawapo ya magari laini ya Nissan yenye umbo dogo ila imejaa mifumo ya usalama.

3

Hii gari ilianzishwa kuja kupambana na soko la Subaru Forester na Honda CRV kama Sport Utility Vehicle ikimaanisha gari kwa matumizi ya barababra zisizo rasmi. Kuna Nissan X-Trail T30, T31 na T32.

4

Sifa za Nissan X-Trail T30: 1. Kwanza, haijifanyi kuwa chochote ambacho sio. Ni gari thabiti, la busara, la vitendo, si la ishara ya hali ya uso wako.

5

2. Ni gari bora lakuaminika, linaheshima kuendeshwa barabarani na ni bora katika makundi ya magari yanayoweza kutumika katika barabara zisizo rasmi.

6

3. Ni bora pale matumizi ya mwendo ya matairi manne (4x4) yanapohitajika badala ya mitindo ya muonekano wa gari.

7

4. Ni gari la bei rahisi ukilinganisha na magari ya kundi lake kwa matumizi ya barabara zisizo rasmi (SUVs). Gari hizo ni kama Rav4, Subaru Forester, Honda CRV.

8

5. Ni gari la heshima kwaajili ya familia. Lina nafasi kubwa kwa nyuma kwa kukaa watu na sehemu ya mizigo kubwa iliyotengenezwa kwa plastiki ili iwe rahisi kusafisha ikichafuka.

9

6. Kioo chake cha mbele chenye mlalo mkali na vioo vyake vya pembeni vilivyosimama wima, vimethibitisha urithi wake kwa matumizi ya barabara zisizo rasmi.

10