1
Mwaka jana, kuna wakati tuliongelea kuhusu ushindani kwenye biashara. Wakati huo, tiliona kuna changamoto kwenye uelewa wa watu juu ya maana halisi ya mshindani kwenye biashara. Tuangalie tena maada hii...
2
Wengi Tunavyofikiri. Kwa haraka haraka, tukiambiwa, 'Mshindani kwenye biashara', tunaanza kufikiria biashara zote ambazo zinafanana na biashara zetu.
3
Ni Kweli. Biashara zinazo fanana na biashara zetu, ni washindani wetu. Lakini ushindani kwenye biashara unaenda zaidi ya hapo.
4
Maana Ya Mshindani Kwenye Biashara. Kitu au mtu yeyote atakaye mfnaya mteja asije kwako, kupata huduma.
5
Kwa Mfano. Ifuatayo ni mifano mbalimbali za biashara ambazo zinashindania wateja, bila kuwa wazi sana kwa watu.
6
Mgahawa na Gym. Mteja wa gym anaweza kushauriwa asiende mgahawa fulani kula kitu fulani ili apunguze uzito.
7
Comments