1
Michezo ni afya, michezo ni taaluma, michezo ni burudani kwa watoto. Michezo ina umuhimu katika ukuaji wa watoto kama kilivyo chakula katika mwili. Kutothamini michezo ni kutomthamini mtoto.
2
Baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa na utamaduni wa kutothamini michezo kwa watoto na kuona suala la mtoto kucheza ni suala la kupoteza wakati wala halina faida yoyote ile katika makuzi ya mtoto.
3
Uelewa huo sio sahihi hata kidogo, michezo inafaida nyingi sana kwa mtoto na wanasaikolojia wanasema mtoto anahitaji lisaa limoja hadi mawili kwa siku katika mchezo au michezo yake.
4
Mzazi au mlezi anahitajika kuwa karibu kwa ajili ya kutizama aina ya mchezo kama nitakavyoeleza hapo baadae, usalama wa mtoto na kuanza kufatilia kipaji chake.Leo tutaangalia aina sita za michezo.
5
19
3
23
5
Comments