KITU MUHIMU ZAIDI KUJUA KATIKA MAHUSIANO

1

Mahusaino ni kama injini. Hakuna uzuri au ubaya unaoweza kujitafsiri wenyewe nje ya mahusiano. Kuhusiana ni hitaji la msingi na muhimu kwa kila mtu hata kama ni mbaya kiasi gani. MAHUSIANO YANA NGUVU!!!

2

Katika kuhusiana, ni lazima kujua kuwa wewe sio kila mtu na ya kwamba kila mtu utakaehusiana nae ana jambo lake ambalo ndilo haswa msukumo wa kuwa karibu au mbali na wewe. MAHUSIANO YANGU NGUVU SANA.

3

Najua kuwa kuna mambo mengi sana ya kujua kuhusu mtu unaetaka kuhusiana nae au ambae unahusiana nae hata sasa ila leo nakuletea jambo moja kubwa kuliko yote ambalo ndilo mzizi mkuu wa uzuri au ubaya.

4

Napenda ujue kuwa MTU NI NIA YAKE. Jambo muhimu zaidi kujua na kulipa heshima yake ni NIA YA MTU. Hili neno NIA NDIO UTU WA NDANI WA MTU. Hakuna mtu anaweza kuwa mzuri au mbaya kuliko au zaidi ya NIA.

5