USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO

1

Fedha inahitaji usimamizi wa hali ya juu ili iweze kuongezeka na kutimiza malengo ulionayo katika biashara yako. Kabla ya kujiuliza fedha zako zimekwenda wapi ni busara kuwa na ujuzi wa kuzisimamia.

2

Unapokosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha inaweza kuzalisha changamoto kadha wa kadha katika biashara yako. Baadhi ya changamoto zinaweza kutokea kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri wa fedha.

3

Changamoto hizo ni kama vifuatazo Unaweza kupata hasara katika biashara yako. Unaweza kupunguza kiasi cha mtaji wako. Unaweza kuingia kwenye mgogoro wa madeni.

4

Unaweza kushindwa kununua mali ghafi kwaajili ya uzalishaji. Unaweza kupoteza thamani ya jina la biashara yako. Unaweza kupunguza thamani ya ubora wa bidhaa zako.

5

Kuna changamoto lukuki ambazo zinaweza kujitokeza kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha hivyo elimu ya masuala ya usimamizi wa fedha ni muhimu sana katika biashara yako.

6