1
Mwisho wa sehemu hii tutajifunza:- > Umuhimu - wa kuelewa kwanini unahitaji nembo - utambulisho wa brand yako(brand identity) - wa msukumo(inspiration) katika kuunda Logo yako.
2
1. ELEWA KWANINI UNAHITAJI NEMBO Unapoamua kuunda logo, unajaribu kuwavuta watu sahihi kwako na kuwafanya waipende brand yako. Nembo yako itawavuta watu sahihi kwako au kuwakimbiza mbali.
3
Logo yako itatoa taarifa za awali kuhusu biashara yako, hivyo itakua na athari kubwa kwa hisia za awali za wateja wako na kuwafahamisha ikiwa itawafaa au lah.
4
Logo yako ni sehemu muhimu sana ya brand yako. Nyenzo zako zote(marketing materials) kuanzia tovuti, vifungashio mpaka kadi za biashara zitakua na logo yako.
5
MUHIMU Ifikirie logo yako kama picha katika wasifu wako itakayofanya watu wapendezwe na kujaribu kujifunza zaidi kuhusu brand yako. Jaribu kuwa katika hali itakayomvutia unaetamani aipende brand yako.
6
MUHIMU. Muundo mzuri wa logo sio tu utawasilisha kile brand yako inakisimamia bali pia huleta hisia nzuri za awali na kukufanya uonekane zaidi miongoni mwa washindani wako.
7
2. BAINISHA UTAMBULISHO WA BRAND YAKO(BRAND IDENTITY). >Kwanini tulianza biashara hii? >Je, imani na maadili kama ni muhimu kwetu kama kampuni? >Nini kinatufanya kuwa maalum?
8
23
4
15
3
Comments