FIKIRI NJE YA TOYOTA

1

Ni wakati sasa wa pale tunapotaka kununua gari kufikiria nje ya Toyota. Magari ya Toyota yamekua yakitawala nchini mwetu, Ila pia Kuna magari imara na mazuri nje ya Toyota. Karibu ujue kwanini.

2

UTANGULIZI: Kwanza kabisa Ni vizuri ujue makampuni ya magari mengine nje ya Toyota yamefanya mapinduzi makubwa kushindana na Toyota katika soko la Afrika.

3

Karibu kwanza tuanze kuangalia kwanini makampuni ya magari nje ya Toyota yalikua hayanunuliwi sana nchini mwetu.

4

1. Teknolojia ya magari mengine ilikua ngeni kwa mafundi. Injini na mfumo wa magari mengine ni tofauti na magari ya Toyota na mashine za Diagnosis zilikua hadimu ivyo kuleta ugumu kwa mafundi.

5

2. Spare za magari ya makampuni mengine zilikua hadimu. Kwasababu magari ya makampuni mengine yameanza kuingia nchini kwa Kasi, wafanya biashara pia wamekua wakizileta spare zake.

6

Na sasa ivi Dunia ni kama kijiji, unaweza agiza spare sehemu yoyote Duniani. Hivyo kwasasa spare zake zinapatikana.

7

3. Bei zake zilikua juu. Saivi bei zake zimeshuka kuliko hata Toyota.

8

4. Magari ya makampuni mengine yalikua mayai sana. Yaani yalikua hayawezi kupambana na mazingira yetu, hitilafu zilikua za hapa na pale.

9

KWANINI UNUNUE MAGARI YA MAKAMPUNI MENGINE ZAIDI YA TOYOTA?

10

1. Spare zake Ni Imara na zina ubora. Makampuni mengine zaidi ya Toyota yamekua yakitengeneza gari na spare zake. Toyota wamekua wakitoa kibali kwa makampuni mengine kutengeneza spare.

11