1
MAAMUZI Kiongozi yoyote ni lazima awe na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi yenye tija kwaajili ya taasisi na watu anaowaongozo.
2
Kuna mambo mengi katika mchakato wa kuongoza yatahitaji kufanya maamuzi. Kama unaongoza kampuni ni lazima ufanye maamuzi kuhusu uwekezaji, miundo mbinu ya kampuni na namna ya kusimamia rasimali.
3
Kufanya maamuzi ni sehemu ya maisha ya kiongozi hivyo ni busara kujua namna bora ya kufanya maamuzi ili kuleta tija katika taasisi anayoingoza.
4
Matarajio ni kuona maamuzi ya kiongozi yaliyopevuka (matured decision), maamuzi yenye hekima, maamuzi yenye weledi na ujuzi.
5
Kuna maamuzi magumu kiongozi anaweza kuhitaji kufanya ili kuhakikisha sera, taratubu na maono ya taasisi yanafikiwa.
6
Kulinga na unyeti wa suala la maamuzi linamhitaji kiongozi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi bora na yenye tija. Uamuzi anaoufanya kiongozi kiongozi unaweza kujenga au kuharibu taasisi.
7
Moja ya namna bora ya kiongozi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ni kuwa na maarifa. Maarifa anayotakiwa kuwa nayo kiongozi ni maarifa mbalimbali sio katika eneo lake la taaluma tu.
8
Maarifa ni mkusanyiko wa taarifa mbalimbali. Kama kiongozi ni lazima kuwa kuwekeza katika kijifunza mambo mbalimbali ili kujenga uelewa mpana.
9
Kama kiongozi ni lazima kujua sera za taasisi, maono ya taasisi na mambo mengine yanayohusiana na taasisi husika ili maamuzi yako yasikinzane na taratibu za taasisi.
10
9
2
18
4
R
Ritha Mallya
Nice course, very educative. Few spelling mistakes to be attended on.
Comments