1
Tutajifunza; 1. Manufaa ya kusoma vitabu. 2. Hasara za kuto kusoma vitabu. 3. Jinsi ya kujifunza kusoma vitabu.
2
Kuficha Maarifa. Kuna msemo unasema, ukitaka kumficha mwafrika taarifa au ujuzi fulani basi ufiche kwenye vitabu...
3
Msemo huu huwa unasemwa kumaanisha kwamba asilimiakubwa ya waafrika hatupendi sana kusoma vitabu.
4
Hali Halisi. Ni kweli kwamba asilimia kubwa ya Waafrika hatupendelei sana kusoma vitabu. Na kuna sababu nyingi ambazo zinazopelekea kitu kama hichi kutokea.
5
Tamaduni Zetu. Sababu kuu ya kuwafanya watu wengi hapa Afrika wasipendelee kusoma vitabu ni tamaduni.
6
Kwa haraka haraka tu, ukiangalia watu wengi wanao penda kusoma vitabu, utakuta walijengewa tabia hizi tangu wakiwa watoto.
7
Lakini asilimia kubwa ya watoto wa kiafrika wanakuzwa bila kuwa na tamaduni za kusoma vitabu. Hata ukiangalia michezo ambazo wanacheza sio ambazo zinahitaji mtoto asome sana.
8
Hatari kubwa zaidi kwa kizazi cha sasa ni pale wazazi wanavyo waachilia watoto kuangalia katuni kwenye simu zaidi kuliko kuwajengea tabia za kusoma zaidi.
9
Utandawazi.π Kati ya vitu ambavyo vinaonekana kubadilika kutokana na utandawazi ni jinsi ambavyo taarifa nyingi zimekuwa rahisi kupatikana.
10
Utandawazi umefanya upatikanaji wa taarifa mbalimbali pamoja na vitu kama vitabu kuwa rahisi kupatikana.
11
Changamoto Iliyobaki. Kwa tulipofikia, upatikanaji wa vitabu vya aina mbalimbali, aidha vitabu vya karatasi (hard copy) au vitabu vya digitali (soft copy) vyote ni rahisi kupatikana. Lakini changamoto iliyopo ni ile ya tamaduni.
12
Inaonekana hata kama ukimpa mtu kitabu cha bure, bado ni ngumu kwake kujitengenezea mazingira ya kusoma vitabu hivyo.
13
Tujenge Tabia. Njia mmoja wapo ya kuanza kutengeneza mazingira ya kusoma vitabu inaweza kuanzia kwenye kuelewa manufaa yaliyipo kwenye kusoma vitabu.
14
Manufaa Ya Kusoma Vitabu. - Kuchangamsha akili. - Kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu zaidi. - Kuwa mbunifu zaidi.
15
49
23
28
6
Comments