Sehemu ya Pili - Jinsi ya kuboresha uhusiano wako na pesa!

1

Huu ni muendelezo wa sehemu ya kwanza. Tutakumbushana: 3. Mahusiano yetu ya mwanzo kabisa na pesa 4. Jinsi ya kutibu mahusiano mabaya na pesa 5. Jinsi ya kuboresha mahusiano na pesa

2

3. Mahusiano yetu ya mwanzo kabisa na pesa Je ulifanikiwa kufanya zoezi la kufuatilia kuhusu siku yako na jinsi ulivyohusiana na pesa. Aidha kwa kufanya miamala mbalimbali au kuizungumzia?

3

Umepata majibu gani? Ni upande gani wa jedwali lako umeelemea? wa hisia hasi au chanya? Hii ni hatua ya kwanza ya kupima uhusiano wako na pesa.

4

Pia ni kipimo bora cha kukuonyesha athari ya taarifa ulizopata awali kabisa kuhusu pesa. Wapo tulioambiwa kuwa pesa ni chanzo cha matatizo yote. Wapo tulioshuhudia hilo kwa kuona labda watu wakipoteza maisha kwa kukosa pesa ya matibabu.

5